TANGAZO LA KAZI

IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER ANAPENDA KUTANGA NAFSI YA KAZI MTECHINOLOGIA MAABARA KWA KUSIMAMIA MAABARA

IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER.

Mkataba huu umefanyika leo TAREHE……MWEZI……MWAKA 20…..
KATI YA
IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER yenye usajili namba……..
Ni HEALTH LABORATORY CENTER inayotoa huduma za afya (vipimo) katika kijiji cha ugansa , wilaya ya kaliua mkoa wa tabora.
NA
Ndugu……………………………wa S.L.P………wilaya………..mkoa……………Mawasiliono namba…………………..Ambaye atajulikana kama MWAJILIWA kwa upande mwingine.
Wakati MWAJIRI ameonyesha nia ya kumuajiri katika kituo hiki cha afya(vipimo), Na wakati MWAJILIWA amekubali Kuajiliwa na kufanya kazi kwa IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER.
BASI INASHUHUDIWA NA KUKUBALIWA NA PANDE ZOTE MBILI KAMA IFUATAVYO:
A: WAJIBU WA MWAJIRI
Kulipa mshahara kila mwezi kulingana na makubaliano.
Atatoa likizo moja ya siku 28 kila mwaka au likizo ya kila miezi mitatu na sivinginevo.
Atatoa matibabu bule kwa mwajiliwa mme na mke,ambayo yanapatikana kituoni na yale yanayopatikana nje ya kituo.Lakini mwajiliwa anapaswa kujiunga na mufuko wa Bima ya afya.
Mwajiri atasimamia sheria na kushirikiana na kamati ya mabolesho ya sekta hii (uality Improvement Team).
Mwajiliwa atakuwa chini ya uangalizi wa miezi sita kabla ya kuthibitishwa kazini Matazamio yatahusu utendaji wake wa kazi na mwenendo mzima katika kupenda , kubuni na kutekeleza majukumu yake ya kila siku,Endapo mwajiri hataridhishwa na utendaji wake katika kipindi alichotaja mwajiri hata sita kushirikiana na kamati ya maendeleo,kukutoa au kukuondoa kulingana na sheria na taratibu zilizowekwa na kamati hiyo.
B. WAJIBU WA MWAJILIWA.
Kuwahi kazini ni saa 1:30 Am asubuhi, kufanaya kazi kwa bidii na kujiamini bila kusimamiwa.
Kutotumia kilevi cha aina yoyote ile kama vile pombe na madawa ya kulevya kwenye mudaa wa kufanya kazi.
Kufanya kazi kwa uadilifu ,ubunifu ikiwa ni pamoja na kutunza mali ,vifaa na majengo.Kumbuka mkosa ya wizi au uharibifu wa mali yoyote ile sheria kali itachukuliwa dhidi yako.
Kutoa taarifa kwa uongozi kama unatoka nje ya eneo la kazi,kama hutofanya hivyo yakupasa kuwepo kazini mdaa wote.
Kuwa nadhifu wewe binafsi na mazingira yanayokuzunguka kazini na kuvaa sare muda wa kazi mfano LABORATORY COAT.
Kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa au wateja na wafanyakazi wengine. Lugha ya mtusi na ugomvi kazini haviruhusiwi.
Kuzingatia taratibu na maadali za taaluma za afya(kutokutoa siri za wagonjwa,kutofanya migomo baridi)kwani hayo hupunguza ufanisi wa kazi.
Kutoa taarifa kabla ya miezi mitatu (3) kabla ya kuacha kazi kwa sababu zako binafsi.utarudisha mushahara wa mwezi mmoja iwapo utaamua kuacha kazi ndani ya masaa 24 kwa sababu zako mwenyewe.
Utapangiwa kazi nyingine pindi mwajiri atakapo ona unauwezo wa kufanya hiyo kazi iliyokusudiwa wakati wowote itakapo bidi kufanya hivyo.
HUDUMA ZITOLEWAWAZO IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER
Zifuatazo ni huduma zitolewazo ,Ambazo mwajiliwa atawajibika kulingana na masitahiki yake na ujuzi alionao:
Uchunguzi wa maabara(LABORATORY INVESTIGATION)
Ushauri nasaha wa vipimo.
HIVYO BASI Mwajiliwa nimekubali KUAJILIWA na IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER katika nafasi ya………………………..kwa malipo ya Tsh………………………..kwa mwezi na niko tayali kufanya kazi kulingana na miongozo ya wizara ya afya.
Mkataba huu utadumu kwa muda wa MIAKA/MWAKA………………..
Kuanzia TAREHE…………MWEZI…………MWAKA 20…………..
Mpaka TAREHE……………MWEZI…………MWAKA 20…………
INAKUBALIWA NA KUSHUHUDIWA ZAIDI YA PANDE ZOTE MBILI KAMA IFUATAVYO:
Mwajiri na mwajiliwa tunathibitisha kwamba tumekubaliana na vifungu hivyo vya mkataba huu na kutia saini zetu kama inavyoonyesha hapo chini na katika muda na siku zilizotajwa hapo juu.
Mkataba huu umetiwa sahihi na MWAJIRI, IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER Ndugu jina………………………………SAHIHI………CHEO……………………..MWAJIRI
LEO TAREHE………MWEZI……….MWAKA 20……………..

Mkataba huu umetiwa sahihi na MWAJILIWA wa IGOYE HEALTH LABORATORY CENTER Ndugu………………………………SAHIHI………CHEO……………………MWAJIRIWA LEO TAREHE………………MWEZI…………….MWAKA 20…………..

Maombi yaambatanishwe na mkataba huu maombi yatumwe kwenye namba ya simu hapo Kwenye mkataba au hii 0626349773

eldadlichard@gmail.com

Leave a Comment